Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga bila Fei Toto ni moto!

Fei Toto Asd.jpeg Fei Toto

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Desemba 23, 2022, zilitoka taarifa za Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuandika barua ya kuvunja mkataba wa kuitumikia Yanga, kisha kurudisha fedha kiasi cha shilingi milioni 112 ili kutimiza takwa la kuvunja mkataba huo.

Kesho yake kwa maana ya Desemba 24, 2022, mwenyewe aliaga rasmi ndani ya Yanga kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Fei Toto aliyeanza kuitumikia Yanga 2018, aliandika hivi: “Umekuwa wakati mzuri sana kuichezea Klabu ya Yanga, klabu yenye historia kubwa na ya kuvutia nchini na Afrika yote.

“Tumekuwa na nyakati nyingi mchanganyiko, tulifurahi pamoja pale furaha ilipokuja uelekeo wetu na tulihuzunika pamoja nyakati mbaya zilipotutokea. “Nitakumbuka mengi mazuri yaliyotutokea pamoja na nitasahau yote mabaya kwa haraka sana.

“Kila nikiwakumbuka mashabiki wa Wananchi moyo unakuwa mzito kuwaaga, hivyohivyo kwa wachezaji wenzangu na viongozi pia kwa upendo mlionionyesha tukiwa pamoja kwenye shida na raha. Lakini lisilo budi hutendwa au hunenwa kwa hiyo leo nasema kwaherini Wananchi.

“Ila maisha ndivyo yalivyo mambo huja na kupita na kuna wakati yanajirudia, mpaka wakati mwingine tena. Kwaheri ya kuonana.”

Tangu hapo, kumekuwa na sarakasi nyingi, Yanga wakaenda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufungua shauri la kupinga uamuzi huo wa Fei Toto, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ikamuamuru mchezaji huyo arudi Yanga kwani bado ni mchezaji halali wa timu hiyo, hata alipoomba marejea ya shauri hilo, aligonga mwamba.

Hivi karibuni, Fei Toto alienda TFF kuwasilisha barua rasmi ya kuvunja mkataba huo, hivyo majibu yanasubiriwa nini kitaamuliwa.

Ukichana na hilo, rekodi zinaonesha kwamba, Fei Toto tangu acheze mechi yake ya mwisho ndani ya Yanga Desemba 20, 2022 dhidi ya Coastal Union siku ambayo alifunga bao la mwisho wakishinda 3-0 Uwanja wa Mkapa, Dar, timu hiyo imecheza mechi 13 za kimashindano.

Katika mechi hizo, Yanga imeshinda 10, sare 2 na kupoteza 1, huku ikifunga mabao 24 na kuruhusu 7. Imekusanya pointi 32 kati ya 39 na clean sheet 9.

Ukichukua rekodi za mechi hizo 13 baada ya Fei Toto kuondoka ukilinganisha na zile 13 za kwanza wakati yupo Yanga msimu huu, unaona kuna tofauti kubwa sana.

Rekodi zinaonesha kwamba, mechi 13 za kwanza wakati Fei Toto yupo Yanga, timu hiyo imekuwa na rekodi nzuri zaidi ya wakati huu hayupo.

Ipo hivi; Mechi 13 za kwanza, Yanga ilifunga mabao 26, ikaruhusu 8. Imeshinda mechi 9, sare 3, imepoteza 1. Pointi ilizokusanya ni 30 kati ya 39, huku clean sheet zikiwa 5.

Kwa jumla wakati Fei Toto akiwa Yanga tangu kuanza kwa msimu huu katika michuano yote, timu hiyo imecheza mechi 24, imeshinda 18, imepoteza 2, sare 4. Imefunga mabao 54, imeruhusu mabao 10, clean sheet zikiwa 16 na kukusanya pointi 58.

13 ZA KWANZA FEI TOTO AKIWEPO MECHI: 13 USHINDI: 9 SARE: 3 KUPOTEZA: 1 MABAO YA KUFUNGA: 26 MABAO YA KUFUNGWA: 8 CLEAN SHEET: 5 POINTI: 30

BILA YA FEI TOTO MECHI: 13 USHINDI: 10 SARE: 2 KUPOTEZA: 1 MABAO YA KUFUNGA: 24 MABAO YA KUFUNGWA: 7 CLEAN SHEET: 9 POINTI: 32

JUMLA ALIZOKUWEPO FEI TOTO MECHI: 24 USHINDI: 18 KUPOTEZA: 2 SARE: 4 MABAO YA KUFUNGA: 54 MABAO YA KUFUNGWA: 10 CLEAN SHEET: 16 POINTI: 58 Makala

Chanzo: www.tanzaniaweb.live