Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga bado wawili, kuanza kambi leo Dar

Prince Dube M 1024x819.jpeg Yanga bado wawili, kuanza kambi leo Dar

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga inajiandaa kuingia kambini leo Jumatatu pale Avic Town, jijini Dar es Salaa, lakini ukweli ni kwamba haijamaliza kazi katika kusuka kikosi chao cha msimu ujao na baada ya kumtangaza straika wa zamani wa Highlanders ya Zimbabwe na Azam FC, Prince Dube juzi usiku kwani kuna mashine moja ilikuwa iwekwe wazi jana ila kazi bado inaendelea.

Yanga jana ilitarajiwa kumtambulisha beki mpya wa kushoto, Chadrack Boka aliyepo nchini tayari kwa kuanza kazi akitokea FC Lupopo ya nchini kwao, DR Congo. Boka anakuja kuchukua nafasi ya Mkongomani mwenzake Joyce Lomalisa ambaye mabosi wa Yanga wanataka safari yake iishie hapa kufuatia mkataba wake kumalizika.

WINGA Hata hivyo, taarifa ambazo Mwanaspoti imezinasa ni kwamba ukiondoa Boka umesalia utambulisho mmoja tu wa staa aliyesaini ambaye ni straika Jean Baleke.

Ukiacha hao, Yanga bado inasaka saini mbili za mwisho akiwemo winga mmoja wa kazi anamudukutokea kulia na kushoto, kufuatia klabu hiyo kusitisha kumchukua Manu Lobota.

Mabosi wa Yanga bado wamemganda winga Phillipe Kinzumbi na sasa inasaka usahihi wa mkataba alionao baada ya awali  kuwaeleza kuwa amemaliza mkataba aliokuwa nao na klabu ya Mazembe, japo klabu hiyo ikidai bado ana mwaka mmoja.

Ukiacha Kinzumbi ambaye awali ilivuma kwamba anakwenda Morocco, lakini hilo likakwama, Yanga pia inamsubiri winga Agee Basiala ambaye wiki hii atatua na kikosi chake cha AS Union Maniema.

Maniema inakuja kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya hapa nchini na kuna uwezekano mkubwa ikaishi pale AVIC Town, ambapo mabosi wa Yanga wanataka kumsoma pia kwa mara ya pili kabla ya kuamua kumbeba jumla.

MRITHI WA AUCHO Ukiacha nafasi ya winga pia Yanga inafikiria kumsaka kiungo mmoja wa maana wa kati ikitaka kuanza kujiandaa na maisha bila Khalid Aucho, ikitambua kwamba endapo Mganda huyo akikosekana kikosi chao hukosa nguvu kubwa.

Tayari Yanga imeshamtosa njiani kiungo Gift Mauya aliyesajiliwa na Singida Black Stars baada ya mkataba wake kumalizika kisha usajili wa Yusuf  Kagoma kuingia mwiba.

Yanga inataka kumuangalia kiungo mwingine Onoya Sangana hapohapo Maniema, ingawa tayari mabosi wa mabingwa hao wa Tanzania wameshaambiwa jamaa anajua lakini bado anatakiwa kusalia akomae zaidi.

“Timu inaingia kambini, lakini zoezi la kushusha mashine za kukiongezea nguvu kikosi inaendelea, yaani ni weka niweke hadi kieleweke tena kwa msimu ujao wa mashindano, kwani Wananchi tumepania,” alisema mmoja wa vigogo wa klabu hiyo inayoshikilia mataji 30 ya Ligi kuu Bara tangu ligi hiyo ilipoasisiwa mnamo mwaka 1965, ikifuatiwa na Simba yenye 22.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live