Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga bado wamo CAF, Azam yang'oka

77665 YANGAA+PIC

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

YANGA imeondolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Zesco United mchezo wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Levy Mwanawasa, mjini Ndola Zambia.

Kwa matokeo hayo Yanga wanaenda kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika huku wakisubiri kucheza kati ya Proline (Uganda), Triangle United (Zimbabwe), TS Galaxy FC (Afrika Kusini) au Zanaco (Zambia).

Kipindi cha pili dakika ya 51, Zesco walikosa goli baada ya Jesse Were kupiga pasi mpenyezo ndani ya boksi na kukutana na Weston Kalengo ambaye aliupiga mpira lakini kipa Metacha Mnata alikuwa ameshatokea na kuucheza mpira huo na kukutana na mshambuliaji wa Zesco ambaye alipiga shuti lakini Kelvin Yondani aliokoa.

Were aliipatia Zesco bao la kwanza dakika ya wakati Yanga ikisawazishiwa na Sadney Urikhob, mabao yote yalifungwa kipindi cha kwanza.

Zesco walikuwa wakitengeneza nafasi nyingi kipindi cha pili baada ya dakika 59, Kalengo kukosa goli baada ya kubinuka tiktaki akitumia vizuri krosi iliyopigwa na John Ching'andu.

Zesco ilifanya mabadiliko dakika 63 alitoka John Chin'andu na kuingia Kondwani mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo.

Dakika 66 Mwira Phiri alipewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Deus Kaseke na kuwa kadi ya kwanza kwa upande wa Zesco United.

Yanga walionekana kulinda goli zaidi kipindi cha pili baada ya kurudi nyuma na kumuacha Sadney mbele pekee yake, lakini hali hiyo iliwafanya Zesco wapeleke mashambulizi zaidi.

Dakika 79, Zesco ilipata goli la pili baada ya Quadri Aladeokun alimtoka kwa kasi beki wa Yanga, Ally Ally na kupita kwa kasi na kupiga krosi ambayo kiungo Abdulaziz Makame alijikuta akiunganisha na kupeleka mpira wavuni (alijifunga).

Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Feisal Salum, Patrick Sibomana na Ally, wakiingia Juma Balinya, Mrisho Ngassa na Maybin Kalengo, mabadiliko hayo yalionyesha dhahiri kuongeza kasi katika nafasi ya ushambuliaji.

Dakika 90+  beki wa Yanga, Lamine Moro alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Zesco Utd, Kalengo, Moro alipewa kadi nyekundu kwa kucheza faulo hiyo ambapo awali tayari alikuwa na kadi ya njano.

Kwa upande wa Azam FC imeondolewa katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Triangle United ya  Zimbabwe. Bao la Triangle lilifungwa na Trevor Mahvunga.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Chamazi jijini Dar es Salaam, Azam FC ilikubali kipigo cha bao 1-0 hivyo kuondolewa kwa jumla ya mabao 2-0.

MATOKEO MENGINE

Proline 2-1 As Kigali

Zanaco Fc 3-0 Bolton City

CNaps Sport 1-4 TS Galaxy

 

Chanzo: mwananchi.co.tz