Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga bado nane tu wanabeba tena, Guede wa moto

Aziz Guedee WA0014 Yanga bado nane tu wanabeba tena, Guede wa moto

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bado pointi nane tu kwa timu ya Young Africans SC kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mashujaa.

Joseph Guede ndiye aliyetupatia ushindi huo baada ya kufunga dakika ya ya 41 akimalizia pasi ya Mudathir Yahya, mchezo ukipigwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Hilo linakuwa goli la tano kwa Joseph Guede kwenye ligi msimu huu baada ya kujiunga na Young Africans katika usajili wa dirisha dogo.

Ushindi huo unaifanya Young Africans kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 65, zikisalia mechi tano kuhitimisha msimu.

Katika mechi hizo tano zenye pointi 15, tunahitaji pointi nane ili kufikisha 73 ambazo hazitaweza kufikiwa na wapinzani wetu jambo ambalo litatufanya tutetee ubingwa wetu.

Ubingwa wa msimu huu utakuwa wa 30 kwetu tukiendelea kuwa mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania.

Msimu huu katika mechi mbili tulizocheza dhidi ya Mashujaa nyumbani na ugenini, tumeshinda zote, ya kwanza ilikuwa 2-1, kisha 1-0.

Mechi tano zilizosalia ni dhidi ya Kagera Sugar (nyumbani), Mtibwa Sugar (ugenini), Dodoma Jiji (ugenini), Tabora United (nyumbani) na Tanzania Prisons (nyumbani).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live