Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga baba lao, watwaa Ubingwa Azam Sports Federation

Yanga Bingwa Picha Yanga imeshinda kwa bao la Kennedy Musonda

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Tanzania, Yanga wamefanikiwa kutetea mataji yote baada ya jioni hii kutwaa pia na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Shujaa wa Yanga leo ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 14 akimalizia kazi nzuri ya beki Mkongo, Djuma Shabani.

Pamoja na ubingwa wa Ligi Kuu na ASFC, Yanga pia ni washindi wa Ngao ya Jamii na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika, wakihitimisha msimu mzuri kwao kihistoria chini ya kocha Mtunisia, Nasredeen Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: