Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga asipozuiwa atabeba tena

Ubingwa Ligi Kuu Yangaaa Yanga asipozuiwa atabeba tena

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa sasa Yanga iko kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC wakiwa na alama 43 na michezo yao 16 huku Azam FC wao wakiwa nafasi ya pili na alama zao 43 na michezo 18.

Mnyama Simba yupo nafasi ya tatu akiwa na alama zake 36 na michezo 15,kama atashinda mchezo wake wa kiporo atakuwa na alama 39 maana yake alama 4 nyuma ya Yanga.

Moja ya mechi ambazo zinaweza kumzuia Yanga asiwe bingwa msimu huu basi ni mechi mbili ambazo ni mechi ya Azam Machi 17 na ile ya Simba April 18.

Katika hizo mechi mbili kama Simba na Azam FC watashindwa mmoja wapo kumfunga Yanga na mechi nyingine kupata droo basi uwezekano utakuwa mdogo kwa timu nyengine kumzuia Yanga asiwe bingwa msimu huu.

SIMBA NA AZAM FC MKISHINDWA KUMZUIA YANGA ANABEBA UBINGWA WA TATU.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live