Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EA Radio, Justine Kessy amesema kwa asilimia kubwa ni kama Klabu ya Yanga wameimaliza Ligi Kuu ya NBC msimu huu hivyo wanayo nafasi kubwa ya kubebwa ubingwa wa ligi hiyo.
Kessy amesema hayo baada ya wapinzani wa Yanga kwenye mbio za Ubingwa, Simba na Azam Fc kudondosha alama na kuachwa gape kubwa kwenye msimamo wa ligi hiyo.
“Simba wamerejea jana mabao mawili alama tatu, bao la kwanza likifungwa na Fredy na bao la pili likifungwa na Andre Onana. Naona bado mbio sio kubwa kwamba Yanga wameawaacha sana Simba na sioni sehemu ambapo wataenda kuteleza dhidi ya hawa wawili.
“Yanga ana mchezo dhidi ya Simba na mchezo dhidi ya Azam FC, wataweza kuifunga Yanga? Sina uhakika lakini Yanga ana uwezo wa kupata sare dhidi yao kwa asilimia 80 na uhakika wa kumfunga Simba na Azam ni asilimia 60.
“Hapo unaweza kuona Ligi kwa asilimia flani imeshakwisha, ni asilimia 70 mpaka 65 Yanga ameimaliza Ligi na anakwenda kuchukua Ubingwa wa NBC Premier League kwa mara ya tatu mfululizo,” amesema Justine Kessy.