Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga acheni utani, Maxi bilioni 3?

Maxi Mpiah Nzengeli Ms Yanga acheni utani, Maxi bilioni 3?

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi karibuni kumeibuka taarifa za Klabu ya Simba kuhusishwa na usajili wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Max Mpia Nzengeli hasa kuelekea katika ujenzi wa timu yao wakati wa kipindi cha dirisha dogo Januari.

Baada ya uvumi wa taarifa hizo, mmoja wa maafisa ndani ya Klabu ya Yanga, Alex Ngai amesema kuwa thamani ya Maxi Nzengeli sokoni ni Bilioni 3.

Hivi hizo Bilioni mnazitaja tu ama? Hivi mchezaji ambaye hajawahi kushinda kombe lolote ndani ya Yanga anauzwaje Bilioni tatu? Mchezaji ambaye kaanza kujipata akiwa Yanga anauzwaje Bilioni 3?

Acheni hizo ndugu zangu Wananchi, Maxi Mpia Nzengeli hawezi kuwa na thamani hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live