Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Yawaandalia Mikataba Minono Mwamnyeto,Yacouba

YANGA (600 X 472) Yanga Yawaandalia Mikataba Minono Mwamnyeto,Yacouba

Sun, 6 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UONGOZI wa Yanga, umezima tetesi za kuondoka baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na kuweka mazingira ya kuwapa mikataba mirefu.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimesema kuwa: “Ndani ya Yanga hakuna atakayeondoka tena, kwa sababu inataka kujenga timu yenye kikosi kipana, wote ambao mikataba yao ipo ukingoni itaongezwa.”

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro alisema: “Kwa kawaida timu inayotengeneza kikosi bora haiwezi kuacha mchezaji holela.

“Kwa sababu kwa kufanya hivyo inakuwa ni sawa na kurudi nyuma baada ya kwenda mbele, Yanga itawapa mikataba mipya wachezaji wote ambao mikataba yao ipo ukingoni, hakuna atakayeondoka.”

Baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu ni nahodha Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Saidi Ntibazonkiza, Yacouba Songne, Deus Kaseke na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live