Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Vs Simba kamera 111 zitawashwa Uwanja wa Taifa

98356 Kamera+pic Yanga Vs Simba kamera 111 zitawashwa Uwanja wa Taifa

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

ZAIDI ya kamera 100 zitatumika kuimarisha usalama wa watazamaji Uwanja wa Taifa leo Jumapili kwenye mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Simba ambao unategemewa kukusanya idadi kubwa ya watazamaji. Mechi hiyo itapigwa saa 11 jioni huku ikitazamiwa kuingiza mashabiki 60,000 na ushee. Meneja wa uwanja huo, Godwin Nsajigwa alisema mchezo wa dabi unakuwa na mambo mengi na kukutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali, hivyo lazima usalama utazamwe kwa jicho la kipekee. “Uwanja wa Taifa una kamera 111 ambazo siku ya mchezo zitaangaziwa kwa mashabiki ili kulinda mali na usalama wa raia, hivyo nategemea ustaarabu wa kila mmoja. “Zamani kukifanyika uharibifu timu ndio ilikuwa ikiadhibiwa, lakini kwa sasa shabiki atakayebainika atachukuliwa hatua husika na sio timu,” alisema Nsajigwa. Aliongeza kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa kuanzia kurekebisha ndani ya eneo la kuchezea  kwa kuweka dawa ya fangasi na kupunguza urefu wa nyasi. Nsajigwa alisema uwanja unalindwa na ulinzi maalumu, hivyo hawataruhusu kundi lolote kufanya ulinzi eneo la uwanja na ikitokea hivyo watachukuliwa kama wahalifu. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke, Amon Kakwale alisema wamejipanga ndani na nje ya uwanja kuhakikisha usalama unakuwa mzuri kama ilivyokuwa kwenye michezo mingine ya ligi ya ligi. “Usalama utakuwa asilimia 100 na hiyo ndio azma ya Jeshi la Polisi kuhakikisha raia wake wanakuwa katika mazingira salama na rafiki kufurahia mchezo wowote utakaochezwa kwenye viwanja vinavyopatikana Mkoa wa Polisi Temeke,” alisema Kakwale. “Natoa tahadhari kwa wale wenye mihemko ya kishabiki hasa ule ushabiki usiokua na staha na kusababisha fujo hatutasita kuwachukulia hatua kali.” Aliongeza mashabiki wanakuja uwanjani wajitahidi kulinda amani ili furaha ya mchezo izidi kuongezeka hata wanaporudi nyumbani bila kuja matokeo yao ya mchezo.

Chanzo: mwananchi.co.tz