Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Ubingwa tunachukua mapema tu!

Mzize Aucho Fv Yanga: Ubingwa tunachukua mapema tu!

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imesema kuwa licha ya kutoa sare dhidi ya JKT Tanzania, lakini malengo yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC yako palepale na watahakikisha wanaubeba ubingwa huo mapema kabla mechi hazijamalizika.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari Yanga, Ally kamwe wakati akizungumza na wanahabari baada ya mchezo wao dhidi ya JKT kumalizika huku wakiitupia lawama bodi ya Ligi kupanga mchezo wao na JKT Tanzania upigwe katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ulioonekana kuwa na maji na tope.

"Bila shaka umeona Uwanja wa kuchezea hapa Isamuhyo, tunawaachia wenye mamlaka kama wanaona sehemu pitch hii inafaa kuchezea basi tuendelee kutwanga, ndiyo ligi yetu, ndo soka leu, kivyetuvyetu.

“Lakini sisi kama Yanga tunashukuru kwa kupata alama moja dhidi ya mazingira magum,u ya hapa na tunajipanga kwenye mchezo ujao wa Ligi kuu kutetea ubingwa wetu msimu huu.

“Hatujarudi nyuma hata alama moja, tungepoteza ingekuwa mbaya zaidi, kupata alama moja maana yake tumeongeza alama na tunakwenda kupambana kuhakikisha tunautwaa ubingwa mapema zaidi.

“Kuanzia mechi ijayo tutapambana kwa nguvu kubwa kuhakikisha tunapata matokeo kuanzia mchezo ujao na Coastal Union tutaingia ari kubwa ili kurejea kwenye makali yetu," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live