Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga U20 yainyuka Simba U20 mabao 4-0

Yanga U200 Yanga U20 yainyuka Simba U20 mabao 4-0

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Yanga, jana imeibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Simba U-20 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vijana chini ya miaka 20.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Yanga U-20 iliongoza vipindi vyote kwa magoli 2-0.

Kipindi cha kwanza, Willyson Christopher alifunga bao la kwanza na ingizo jipya kwenye kikosi chetu kutoka JKU Zanzibar, Shekhan Khamis, alifunga goli la pili, kabla ya kipindi cha pili Ahmed Fredrick na Ramadhan Hemed kuhitimisha ushindi huo.

Ushindi huo umeifanya Yanga U-20 kufikisha alama 10 baada ya kucheza mechi 7 na kushika nafasi ya nne katika Kundi A la ligi hiyo lenye timu 8.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live