Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tutasajili majina makubwa, wachezaji bora

Pacome Gamondi Maxi Yanga: Tutasajili majina makubwa, wachezaji bora

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imesema kuwa inasubiri ripoti ya kocha wao mkuu, Miguel Gamondi kwa ajili ya kufanya maamuzi ni wachezaji gani waachwe na wachezaji gani waongezwe kwenye kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.

Hayo yamesemwa na Meneja habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati akizungumza kuhusu kuelekea usajili mpya wa msimu ujao huku akisisitiza kuwa nyota wao wanaowahitaji hawataruhusu waondoke hata kama ni biashara.

“Malengo yetu ya msimu ujao tumeshayaainisha ni kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa hasa Klabu Bingwa Barani Afrika, achana na haya ya ndondo cup. Kuyafikia haya malengo lazima tuhakikishe tunasalia na wachezaji wetu bora na tunaongeza nguvu.

“Msimu unaomalizika usajili ambao tuliufanya haukuwa na majina makubwa, tulikuwa na wachezaji bora wengi mfano kina Maxi Nzengeli mpaka wanafika hapa, ni Watanzania wachache walikuwa wanamjua.

“Yao na Pacome walionekana na ASEC Mimosas lakini hawakuwa na majina makubwa ya kushitua bali uwezo wao ndiyo umewashitua Watanzania. Msimu huu kwenye sajili zetu hatuendeshwi na mihemko ya kwenye mitandao wala propaganda za hovyo hovyo.

“Msimu huu sajili zetu nimechungulia kidogo nimeona kuna wachezaji bora wengi wataongezeka na majina makubwa yatakuwepo. Ni majina makubwa kweli ambayo yataingia msimu ujao,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live