Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tutajua huko huko

MAYELE BANGALA.jpeg Bangala na Mayele

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga inashuka uwanjani usiku wa leo kuivaana na Tanzania Prisons katika mechi ya Kombe la ASFC, huku maafande hao wakikaririwa hawautilii maanani sana mchezo huo kwa vile akili zao zipo zaidi Ligi Kuu Bara, lakini wenyeji wamesema watajua huko huko Azam Complex.

Uwanja huo ndio utakaotumikwa kwa mchezo huo wa hatua ya 16 Bora kusaka timu ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho, huku Yanga ikipiga hesabu za kutaka kutetea taji hilo ililolipata msimu uliopita kwa kuitemesha Simba katika nusu fainali na kwenda kubeba kwa kuifunga Coastal Union kwa penalti baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Yanga imefika hatua hiyo ya 16 Bora kwa kuifunga Rhino Rangers kwa mabao 7-0, wakati Prisons ikiitoa Mashujaa ya Kigoma kwa penalti baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 za mechi ya 32 Bora na leo zinakutana kuanzia Saa 1:00 usiku.

Yanga imeupelekea mchezo huo Uwanja wa Azam Complex, kutokana na uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa kwenye ukarabati na ni pambano la pili kwa timu hizo msimu huu, baada ya awali kukutana kwenye Ligi Kuu duru la kwanza na Yanga kushinda bao 1-0.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na kuwa wa mtoano na atakayepoteza mechi basi atakuwa ameaga michuano hiyo, lakini Yanga ikitaka kutetea taji na Prisons ikitaka kupenya ili kufika mbalio na kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Ubora wa vikosi vya timu zote mbili huenda ukachangia mechi hiyo kuwa bora kwani Yanga imekuwa na kikosi bora katika misimu miwili sasa mfululizo huku Prisons ikiwa na wachezaji wa kiwango cha kati lakini wenye morali ya upambanaji zaidi.

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizi mbili kukutana kwenye hatua hii, lakini bado rekodi katika mechi za Ligi Kuu zinaonyesha Yanga na Prisons zikikutana mechi huwa ngumu kwa pande zote licha ya kwamba Wananchi wameshinda nyingi kuliko Wajelajela.

Katika mechi tano za mwisho Yanga ilipokutana na Prisons kwenye ligi, tatu zilimalizika kwa sare na mbili Yanga ikashinda na zote mbili imeshinda kwa wastani wa bao moja tu, ikiwa ni ile ya Desemba 19, 2021 ambapo Wananchi wakiwa ugenini walishinda 2-1 na nyingine ni ile ya Desemba 4, 2022 Yanga iliposhinda 1-0 kwa Mkapa.

Pamoja na hayo, muenendo wa Yanga kwa siku za hivi karibuni katika michuano yote umeonekana kuwa tishio zaidi ya Prisons kwani katika mechi tano za mwisho imeshinda tatu, kupoteza moja na kutoa sare moja huku Prisons ikiwa haijapata ushindi katika michezo yake mitano iliyopita ya ligi, ikiwa imepoteza minne na kuambulia sare tasa moja.

Kocha mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi alisema wanatambua ni mechi ya mtoano na wanataka kusonga mbele hivyo wataingia uwanjani wakiwaza kushinda tu.

"Prisons imekuwa ikitupa ushindani kila tunapokutana nayo, ni timu nzuri lakini sasa ni hatua ya mtoano hivyo tunahitaji ushindi ili kutetea taji letu na naamini iktakuwa hivyo," alisema Nabi, huku kocha wa Prisons, Abdallah Mohamed 'Bares' alisema licha ya kuwa vibaya kwenye ligi bado ASFC ni michuano mingine na wamejipanga kutoa ushindani kwa Yanga.

Awali kocha huyo alikaririwa na Mwanaspoti kwa sasa akili zao zipo kwenye mechi sita za mwisho za kufungia msimu wa Ligi Kuu Bara ambao wapo nafasi ya 14 na pointi 22, lakini sasa amesisitiza kwa kusema;

"Yanga ipo kwenye ubora, lakini mpira una matokeo tofauti na wengi wanavyotarajia, hatajafanya vizuri katika mechi zilizopita za ligi, lakini sio huku hivyo najua itakuwa mechi ngumu kwetu lakini tumejipanga kupambana na kutafuta ushindi."

Michuano hii ya ASFC ilirejea mwaka 2015-2016 ikiwa na jina hilo kutoka Kombe la FA baada ya kusimama tangu ilipochezwa mara ya mwisho 2002, na huu ni msimu wa saba, huku Simba ikiwa imeshinda mata tatu, Yanga mbili, huku Azam bna Mtibwa Sugar zikiwa zimetwaa mara moja moja.

Mbali na mechi hiyo ya usiku, mapema saa 10:00 jioni itapigwa michezo mingine miwili ya hatua hiyo kwa Geita Gold kuwa wenyeji wa Green Warriors katika Uwanja wa Nyankumbu Geita, huku Singida Big Stars ikiikaribisha JKT Tanzania kwenye Uwanja wa LIti, mkoani Singida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live