Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tutachukua hatua zinazostahili CAF

Ally Kamwe Mpira Ally Kamwe

Sat, 6 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga @alikamwe amesema uongozi wa timu hiyo utachukua hatua juu ya tukio la utata lililotokea jana kwenye mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Katika mchezo huo uliomalizika bila kufungana katika dakika 90, mpira uliopigwa na Stephan Aziz Ki umekuwa gumzo ambapo wengi wanaamini mpira huo ulivuka mstari na kupaswa kuwa goli lakini mwamuzi aliamua tofauti.

Kamwe amewataka Wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho timu yao inaendelea na michuano mingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live