Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tunawataka Simba makundi ya CAFCL

Gamondi Roby Yanga: Tunawataka Simba makundi ya CAFCL

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wanatamani kukutana na watani zao wa jadi, Simba SC kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hii ni baada ya Simba na Yanga zote kwa pamoja kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ambapo yanga iliitoa Al-merrikh ya Sudan huku Simba wakiwatoa Power Dynamos ya Zambia.

Ikumbukwe kuwa, Simba ipo pot namba 2 wakati Yanga Sc wakiwa pot namba 3, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa miamba hao wa soka Tanzania kukutana kwenye hatua hiyo ambapo droo ya kupanga makundi itafanyika Ijumaa ijayo, Oktoba 6, Johannesburg nchini Afrika Kusini.

"Katika kitu ambacho Yanga tunakiombea kwa sasa basi ni kukutana na Makolo kwenye kundi moja la Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Mambo ya uzalendo na kusapotiana tayari yameshamalizika kwenye kufuzu makundi wote tumeingia ila huku kila mtu afe kivyake.

"Maana kwenye timu 15 ambazo zimefuzu hatua ya makundi Makolo peke yao ndio kibonde wetu hivyo tunamtaka.

"Maana tukikutana na makolo kwenye kundi moja tunauhakika wa kuvuna pointi 6 hapo tunakuwa na uhakika wa kufuzu Robo fainali," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live