Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tunawaheshimu Azam ila watatusamehe

Yanga98478 Yanga: Tunawaheshimu Azam ila watatusamehe

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC, utakaopigwa katika Dimba la Mkapa, Jumatatu ijayo Oktoba 23, 2023.



Vijana wa Kocha Miguel Gamondi wapo 'siriazi' kwenye maandalizi hayo kuhakikisha wanaondoka na alama tatu muhimu baada ya kucheza michezo mitano na kupoteza mchezo mmoja mbele ya Ihefu.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Meneja wa Kikosi cha Yanga, Walter Harrison amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wote wamerejea kambini kwa ajili ya kuanza kujiandaa na mchezo huo.

"Tumefurahia kurejea kwenye Uwanja ambao tumekuwa tukicheza soka safi, ninaamini Wananchi wana hamu ya kuiona timu yao ikicheza tena kwenye dimba la Mkapa. Mchezo dhidi ya Azam utakuwa wa kwanza.

"Msimu uliopita michezo yote miwili tuliyocheza na Azam ule wa sare ya bao 2-2 na ule wa bao 3-2 ilikuwa michezo bira kabisa, msimu huu tumewafunga pale Tanga bao 2-0 kwenye Ngao ya Jamii lakini tunapokwenda kucheza nao Jumatatu utakuwa mchezo wa tofauti.

"hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu Azam ni timu bora lakini na sisi tuna timu bora na kila kitu kinaegemea kwetu kwamba tutashinda mchezo huo, ibaki kuwapa heshima wapinzani wetu.

"Timu imeingia kambini leo (jana) kwa ajili ya maandalizi kuekelea mchezo huo mpaka siku ye mchezo wenyewe, mwalimu Gamondi anaandaa mbinu zake pamoja na benchi lake la ufundi ili kuhakikisha wachezaji wanazitumia vizuri na kupata ushindi.

"Wachezaji wote waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa wote wamerejea, bado Aziz Ki peke yake ambaye tunatarajia ataingia kesho (leo), baada ya hapo kikosi kizima kitakuwa kimetimia. Kuongezeka kwa siku moja itatusaidia kuandaa vyema kikosi chetu kwa ajili ya kupata ushindi dhidi ya Azam," amesema Walter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live