Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tunataka kuongoza Kundi

Yanga Cr Belouizdad WA0002 Yanga: Tunataka kuongoza Kundi

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Yanga, kinatarajiwa kuanza safari leo kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Yanga na Ahly ambao wote wameshafuzu hatua ya robo fainali, watakipiga kwenye mchezo huo unaotarajiwa kufanyika Ijumaa, Machi 1, 2024 majira ya saa 1:00 nchini Misri.

“Nimesikia watu wanasema tunakwenda kutalii Misri, ni kweli tumeshafuzu kwenda robo fainali ya CAFCL tukiwa na mchezo mmoja mkononi, sasa huu mchezo bado ni mhimu sana kwetu.

“Kwanza tunataka tuongoze kundi ili hesabu zetu kwenye robo fainali tuanzie away kisha tumalizie nyumbani, kuna faida kubwa ya kuanzia away na kumalizia nyumbani. Msimu uliopita ilitusaidia kwenye Kombe la Shirikisho mpaka tukafika fainali.

“Kama kuna mtu yuko nafasi ya pili, anatakiwa ajue kwamba dhumuni la Yanga kutoka Dar kwenda Cairo ni kukutafuta wewe wa nafasi ya pili, ndiyo dhamira yetu. Tunakwenda kushinda mechi dhidi ya Ahly, hii ni rekodi na si jambo dogo.

“Eng. Hersi aliwaahidi Wanayanga kwamba ataitengeneza Yanga kuwa tishio Afrika, ndicho hiki tunachokiona sasa. Rekodi ambazo yuko nazo Hersi ni kubwa sana lakini bado anaziongeza, kumfunga Ahly kwake itaongeza rekodi," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live