Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tuacheni tutajua huko huko

Yanga Yatua Sudan Yanga: Tuacheni tutajua huko huko

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIKOSI cha Yanga alfajiri ya leo kimepaa kikiwa kamili gado na kutua kiakili Sudan na muda huu tayari kipo Khartoum kikijiandaa na mechi ya kesho dhidi ya wenyeji wao, Al Hilal huku mastaa wa timu hiyo wakisisitiza; “Tutajuana hukohuko.”

Yanga itakaa ndani ya ardhi ya Sudan kwa saa 48 tu na tayari walishatanguliza mashushushu watatu ili kuepuka mizengwe ya nje ya Uwanja.

Imeondoka na majembe 25, sambamba na watu 11 wa benchi la ufundi wakiongozwa na kocha mzoefu wa mji wa Khartoum, Nasreddine Nabi, viongozi na mashabiki 15 kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kuanzia saa 3:00 usiku.

Yanga inahitaji sare ya kuanzia mabao mawili ama ushindi wa aina yoyote ili itinge makundi na kurudia rekodi waliyoiweka mwaka 1998, huku nahodha wa zamani wa timu hiyo, Kelvin Yondani akisisitiza ubora na uzoefu wa baadhi ya mastaa ndio siri ya kuibeba Yanga ugenini.

Yondani akifichua hayo, kipa tegemeo wa timu hiyo, Diarra Djigui aliwahakikisha mashabiki na wanachama wa Jangwani, kwamba wanaenda kusaka matokeo. Kikosi kilichoondoka ni makipa Diarra na Abuutwalib Mshery, huku mabeki wakiwa ni; Djuma Shaban, Kibwana Shomari, David Bryson, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Bakari Nondo, Yanick Bangala na Ibrahim Bacca.

Viungo Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Aziz Ki Stephane, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Farid Mussa, Jesus Moloko, Dickson Ambundo, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’, Denis Nkane, Tuisila Kisinda na Benard Morrison, huku washambuliaji wakiongozwa na Fiston Mayele, Yusuph Athuman na Heritier Makambo.

Kabla ya kuondoka, kipa Diarra aliyefanya kazi kubwa katika mechi ya kwanza, alisema;

“Wao waliweza kutufunga kwetu, kwanini nasi tushindwe kufanya hivyo? Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini hatujakata tamaa kwani bado tuna dakika nyingine 90 muhimu tunawaheshimu wapinzani wetu kwa vile tunawafuata kwao, lakini nawahakikishia mashabiki tumejiandaa kwa ushindani, licha ya kucheza ugenini.”

“Kwa upande wangu, nimejiandaa vyema kuhakikisha naipambania timu ili iweze kufikia malengo ya kutinga hatua ya makundi kama ilivyokuwa mipango yetu tangu tumepata nafasi ya kushiriki, wachezaji wenzangu pia wana hari nzuri ya ushindani tunaomba sapoti ya mashabiki bado tunanafasi.”

MSIKIE YONDANI

“Soka inaamuliwa na dakika 90, Yanga ina dakika 90 nyingine zitakazoamua matokeo kwa ubora wao, mie nawapa asilimia kubwa, wanachotakiwa kuendeleza ubora waliouonyesha hapa kwenye dakika 45 za kipindi cha kwanza na kutumia kila nafasi watakayoipata,” alisema Yondani ambaye ni beki tegemeo wa Geita iliyoondoshwa kwenye hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.

“Mchezo wa Jumapili naufananisha na ule tulioenda kucheza na Al Ahly ya Misri tulioifunga nyumbani bao 1-0 nao wakashinda kwao na kuamuliwa kwa penalti na tukapoteza, Yanga bado ina nafasi kubwa kwa Al Hilal, wakijituma kama tulivyojiamini sisi kipindi kile, kila kitu kuitawezekana.”

Moja ya mtihani wa Kocha Nasreddine Nabi msimu huu ni kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku uongozi ukimsajilia mastaa kibao ikiwemo winga mwenye kasi, Tuisila Kisinda.

Yanga ikishindwa kufuzu kesho itaangukia Playoff za Shirikisho ambazo zitapigwa wiki ya kwanza ya Novemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live