Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: 'Thank You' zinaendelea wiki hii!

Yanga Erd Kikosi cha Yanga

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya yanga, Ally Kamwe amesema kuwa klabu hiyo bado haijamaliza kutangaza wachezaji na viongozi ambao wataachwa na klabu hiyo kuelekea msimu mpya.

Kamwe amesemwa hayo leo Jumatatu, Julai 3, 2023 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar akielezea mambo mbalimbali kuhusu klabu hiyo kuelekea msimu mpya.

“Kuhusu Usajili, tumesikia ‘Thank You’ zimetoka, wanachama wanauliza ‘thank you’ zinaendelea au zimeshamalizika, na haya majembe ambayo yameongezwa, lini tunaanza kuyaona?

“Niwaambie mashabiki na wanachama wa Yanga kuwa, ‘Thank You’ bado hazijafika mwisho, bado zinaendelea.

“Wapo wachezaji baadhi na watendaji kwenye idara tofauti klabu ya Yanga itatangaza kuachana nao ndani ya wiki hii na kuwafungulia fursa ya kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, ndio maana nimesema hii ni wiki ya moto kwelikweli.

Mpaka sasa Yanga imeshaachana na wachezaji wake kadhaa wakiwemo, Tuisila Kisinda, Erick Johora, Dickson Ambundo na Abdallah Shaibu.

Wengine ni Kocha Mkuu Nasreddine Nabi, na kocha wa makipa Mbrazil Milton Nienov.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: