Pengine labda kufungiwa kwa baadhi ya Viongozi wao akiwemo Makamu mwenyekiti Fredrick Mwakalebela, pengine labda kitendo chao cha kugomea mechi yao dhidi ya simba kupigwa muda tofauti na uliokuwa umepangwa awali kulileta hali ya Sintofahamu.
Yanga na TFF hawakuwa katika hali au mahusiano mazuri, na hili lilijionesha katika mazingira mbali mbali.
Lakini kwa sasa haipo hivyo, kila mmoja anashirikiana na mwenzake katika kuendeleza mpira wa nchi hii.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amefunguka na kusema kuwa, kwa sasa Yanga na Shirikisho la Soka nchini TFF wana mahusiano mazuri ya kiutendaji kazi na kuona mchezo wa kiungwana ukionekana kwao.
Mwakalebelea ameyasema hayo wakati alipokuwa anafanya mahojiano na Rais wa Mashabiki, Goza Chuma wa KIPENGA XTRA kipindi namba moja cha michezo cha mashabiki Afrika Mashariki na kati.
“Tuna mahusiano mazuri na shirikisho tunaalikana kwenye shughuli mbalimbali tukituma barua zinashughilikiwa. Majadiliano yetu ya nyuma yamezaa matunda” Amesema Mwakalebela.
Ikumbukwe kuwa Yanga na TFF iliripotiwa kutokuwa na mahusiano mazuri jambo lililopelekea Mhe. Waziri mwenye dhamana ya michezo Innocent Bashungwa kuwataka wawili hao waketi ili waayazungumze na kumalizo tofauti zao mwezi.