Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Singida yoyote anakupiga

Yanga Above Yanga, Singida yoyote anakupiga

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga leo Alhamisi inaikaribisha Singida Big Stars katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na aina ya wachezaji wa timu hizo.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, utaanza saa 1:00 usiku. Yanga inayonolewa na kocha Nasreddine Nabi inaingia kwenye mchezo huo huku mshambuliaji wake Fiston Mayele akiwa na mabao matatu amepoa baada ya kutofunga kwenye mechi tatu mfululizo za mashindano yote.

Upande wa SBS licha ya mshambuliaji wake Meddie Kagere kutokuwa na fomu nzuri akiwa na bao moja tu msimu huu lakini katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Simba, ilibebwa na Deus Kaseke katika sare ya 1-1.

Kwenye mchezo wa nyuma dhidi ya Ihefu Singida ilishinda 1-0 bao lilifungwa na beki Shafiq Batambuze na kwa maana hiyo timu zote zina wachezaji ambao wanaweza kuzipa ushindi timu zao.

Singida ina kiungo Bruno Gomes ambaye ana mabao matatu huku akiwa na uwezo wa kufunga ndani au nje ya boksi.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema wanaenda kucheza na timu yenye wachezaji wazoefu wengi na kocha wao anaijua vizuri Ligi ya Tanzania.

Alisema wanajua ugumu wa mchezo wa leo dhidi ya Singida yenye jina kubwa lakini Yanga ni kubwa zaidi na wanaotakiwa kuhofia ni wapinzani wao na sio wao.

“Hatuchezi kwa ajili ya kutofungwa, tunataka tupate kombe la Ligi, Fa na Mapinduzi pamoja na mengine yote, ukimaliza ligi ukiwa haujafungwa halafu hauna kombe inakuwa haina maana,”alisema Kaze.

Kocha Mkuu wa SBS, Hans Pluijm alisema mchezo wa mpira siku zote ni wa kufanya vitu visivyowezekana kuwezekana hivyo suala la kutofungwa kwa mechi 46 linaweza kumalizika.

“Hili la kutokuwa na wakati mzuri ugenini linaweza kuisha kesho (leo), tunaiheshimu Yanga ila hatuihofii, unacheza na timu kubwa na wewe ukiwa na timu inayoweza kushindana,” alisema Pluijm. Yanga yenye pointi 23 ikicheza mechi tisa kabla ya leo inahitaji ushindi kwenye mchezo huu ili kufikisha pointi 26 na kuishusha Azam inayoongoza ikiwa na pointi 26 ikifungwa 11 wakati Yanga imeruhusu matano.

SBS imepanda Ligi Kuu msimu huu na huu ni mchezo wao wa kwanza kukutana na Yanga.

Chanzo: Mwanaspoti