Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Singida Big Stars ni vita ya wanaume

Yanga ZNZ Kikosi cha Yanga

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna vita kubwa ya soka leo Ijumaa, Januari 6, 2023 visiwani Zanzibar. Yanga dhidi ya Singida Big Stars, huu ni mchezo wa maamuzi.

Nani anafuzu hatua na nusu fainali? Nani anatoka? Timu zote zimefungana pointi kwenye kundi B baada ya kushinda mechi zao za kwanza dhidi ya KMKM.

Tofauti ni kwamba Singida Big Stars wako kileleni kwa faida ya tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mchezo wa kwanza Singida walishinda mabao 2-0 na Yanga wakaichapa KMKM bao 1-0, bao lililofungwa dakika ya mwisho ya mchezo na winga Dickson Ambundo.

Matokeo pekee ambayo Wananchi wanayahitaji leo ni ushindi lakini kwa Singida Big Stars, hata wakipata sare ya aina yoyote, watakuwa na nafasi ya kusonga mbele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live