Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Simba zakumbushwa uswahili

Yanga, Simba Azam Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi.

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limezitaka timu zitakazoshiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao kufanya usajili mzuri kwa ajili ya kufanya vyema katika michuano hiyo na kuipa heshima nchi, imeelezwa.

Mabingwa wa Ligi Kuu, Yanga, Azam FC, Simba zote za Dar es Salaam na Coastal Union ya jijini, Tanga zinatarajiwa kupeperusha bendera ya Tanzania Bara katika mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na kusimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). 

Akizungumza na Nipashe jijini jana, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi, alisema endapo timu hizo hazitafanya usajili bora, zitashindwa kuonyesha ushindani na kufanya vyema katika mashindano hayo.

Madadi alisema anaamini usajili bora utasaidia kuzipa matokeo mazuri na hatimaye kila timu kufikia malengo yake.

"TFF tunazishauri timu zote zinazokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao kuhakikisha zinasajili wachezaji ambao watawapa mafanikio kwa kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa," alisema Madadi. 

Alizipongeza timu zote ambazo zimepata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na kusema wamepata tiketi hiyo kutokana na  juhudi walizozionyesha katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyomalizika mapema wiki hii.

Kiongozi huyo pia amewataka wachezaji wote walioshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Championship kutuma  vizuri muda huu wa mapumziko kwa kufanya mazoezi ya ziada.

Alisema msimu uliopita ulikuwa na msisimko mkubwa kutokana na ushindani ulionyeshwa  na timu zote. 

"Msimu uliopita ulikuwa na ushindani na hali hiyo imefanya ligi yetu kuonekana yenye ubora, vilevile tunawashukuru wadhamini wote kwa kazi nzuri waliyoifanya, " Madai aliongeza.

Mtibwa Sugar na Geita Gold zimeshuka daraja moja kwa moja wakati Tabora United na JKT Tanzania zinasubiri kucheza michezo ya mtoano kwa kupambana na timu kutoka Ligi ya Championship.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live