Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Simba walete wachezaji wakali zaidi ya waliopo - Mshindo

Yanga, Simba Walete Wachezaji Wakali Zaidi Ya Waliopo   Mshindo Yanga, Simba walete wachezaji wakali zaidi ya waliopo - Mshindo

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Mbwana Mshindo amesema Simba na Yanga wanapaswa kuleta wachezaji bora zaidi waliopo ili msimu ujao wafanye vizuri zaidi..

"Yanga kufika hatua ya Robo fainali kwao wamepiga hatua kwa sababu target zao msimu huu ilikuwa ni kufika hatua ya makundi ila kwa Simba wao wamefeli.

"Mnyana Simba amefeli kwa sababu target zake ilikuwa ni kwenda hatua ya Nusu Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL ila hajafanya hivyo.

"Nini kifanyike kuelekea msimu wa mashindano ya Kimataifa? Kikubwa ni eneo la usajili ambapo Simba na Yanga zinapaswa kusajili wachezaji wenye quality zaidi ya hawa waliopo.

"Una Zouzoua Pacome lete mkali zaidi ya Pacome,una Clatous Chama lete mkali zaidi ya Chama.

Kama ukifanikiwa kuleta wachezaji wenye quality zaidi alafu wakina Yao Yao, Max,Aziz Ki na wengine wakaendelea kuwepo haitachukua muda Simba na Yanga kucheza nusu fainali ya CAFCL."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live