Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Simba tutakutana tu!

Simba YangaA0002 Yanga: Simba tutakutana tu!

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa licha ya kufungwa na watani zao Simba Sc kwenye mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii, bado kikosi chao kipo imara na malengo yao msimu huu hayajabadilika.

Kamwe amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa Jumapili wa hatua za awali kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS FC ya Djibouti utakaopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

Katika mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii, Simba na Yanga walitoa sare ndani ya dakika 90, lakini Simba wakaibuka mabingwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-1.

“Wale waliotufunga kwenye Fainali Tanga, tunawaambia kuwa mwezi wa 11 sio mbali sisi ni Binadamu tutakutana na kitaumana,” amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: