Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Simba tuleteeni Mokwena tumalizane naye

Aziz Mokwena 2681708 Kocha Mokwena

Wed, 1 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amewashauri viongozi wa Simba kumsajili kocha Rhulani Mokwena kuchukua mikoba ya Abdelhak Benchikha ambaye amebwaga manyanga na kuondoka klabuni hapo.

Kamwe amesema kuwa wanataka kocha huyo aje Simba ili walipe kisasi baada ya Mamelodi kuwaondoa Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya CAFCL kwa changamoto ya mikwaju ya penati huku bao la Aziz Ki likikataliwa.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza sana viongozi wa Simba, wako very very smart, wanaakili wana brain nzuri ya kujua mpira, yule kocha (Benchikha) alishafika mwisho.

"Lakini sisi kama Yanga tulifurahishwa na maamuzi ya yule kocha kuletwa kwa sababu tulikuwa na kisasi naye, kwa hiyo hawa mabwana kwa sababu wako very smart wakatuletea mtu wetu karibu tukamnyoosha vizuri ameondoka hatudaiani naye.

“Niwaombe viongozi wa Simba watuletee yule kocha wa Mamelodi (Mokwena) na yeye tumalizane naye, wakituletea yule mitano tena wakae madarakani,” Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe.

Itakumbukwa kuwa, Kabla ya kutua Simba, Benchikha alikuwa akiinoa USM Alger ya nyumbani kwao Algeria ambapo alikutana na Yanga kwenye fainali ya CAFCC na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kulingana idadi ya mabao.

Hata hivyo Aprili 20, 2024 Yanga walilipa kisasi kwa Benchikha baada ya kuifunga Simba ya Benchikha mabao 2-1 na ndiyo ilikuwa mechi ya mwisho ya Ligi kwa kocha huyo kabla ya kwenda kwenye michuano ya Muungano Cup na baadae kusepa zake Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live