Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Simba hawachekani usajili mpya - Oscar Oscar

Yanga, Simba Hawachekani Usajili Mpya   Oscar Oscar Yanga, Simba hawachekani usajili mpya - Oscar Oscar

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka la Bongo, Oscar Oscar amesema, Simba SC na Yanga SC hawachekani katika kufanya usajili kwani, wote wamepatia na kukosea.

Oscar amesema, katika wachezaji waliowasajili Simba dirisha kubwa lililopita, walioingia kwenye mfumo ni Che Malone na Fabrice huku upande wa Yanga wakiwa na wachezaji watatu, Yao Kwasi, Max Nzengeli na Pacome.

"Ni kama mashabiki wa Yanga wanaipendelea timu yao ndio maana hatuoni kelele, wameingiza wachezaji watatu tu wa kigeni ambao wameingia kwenye mfumo lakini wengine hawajaingia mpaka sasa.

"Hivyo hivyo Simba, wameingiza wachezaji wapya wengi tu wa kigeni lakini walioingia kwenye mfumo ni Malone na Ngoma, Onana na Miquissone ni kama bado wanajitafuta in, out," alisema Oscar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live