Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Simba hata wakiongoza kwa alama 15, tutawashusha

Ally Kamwe Documentary.jpeg Ally Kamwe.

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa nafasi yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu uko palepale licha ya wapinzani wao Simba Sc kuanza vizuri kwa kushinda katika michezo yao miwili ya mwanzo.

Kamwe amesema hayo jana Jumapili, Agosti 20, 2023 baada ya kumalizika kwa mechi ya Kombe la mabingwa Afrika kati ya ASAS FC ya Djibouti na Yanga ambapo Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0 katika Dimba la Chamazi.

"Kwenye ligi wala hatuna tatizo, hata kama hao wanaoongoza wangecheza michezo mitano mfululizo wakawa na pointi 15, utaratibu wanaujua kwamba pale namba moja kuna mtu anakuja. Kuthibitosha hili ni siku ya Jumatano tutakavyoanza hapa na KMC.

"Kila mtu anawaza kuchukua ubingwa, Mashujaa wanataka ndoo, Ihefu nao wanataka ndoo, Coastal, Singida wote hawa wanataka ubingwa, kimsingi huko ni kujisahau, na KMC ndio watakuwa mfano.

"Kila timu yoyote ikitaka kujaribu ubora wake waje wacheze na Yanga. Washambuliaji wako wakiwa wazuri waje uwajaribu na Yanga, mabeki wako wakiwa vizuri karibu uwajaribu na Yanga, viuongo wako njoo uwajaribu kwa daktari Aucho uone anavyowatibu," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: