Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Simba hakuna mbabe, wageni watakata

B38E1D3E CF7E 4DF3 B384 89000DCDE4E2.jpeg Mchezo umemalizika kwa sare ya goli 1-1

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dakika 90 za Dabi ya Kariakoo zinakamilika kwa sare ya goli 1-1 kati ya vigogo Yanga dhidi ya wekundu wa Msimbazi Simba SC.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam umeshuhudia nyota wapya ndani ya vikosi hivyo wakipachika magoli kwa kila upande.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa nyota wake Augustine Okrah dakika ya 15 akimaliza pasi safi ya Clatous Chama.

Stephen Aziz Ki akaisawazishia Yanga kwa mpira wa adhabu uliojaa wavuni na kumfanya Aishi Manula asijue la kufanya.

Kwa sare hiyo Simba anabaki kileleni ikiwa na alama 14 sawa sawa na Yanga waliopo nafasi ya pili huku Simba wakiwa na faida ya magoli ya kufunga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live