Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Simba, Azam zapewa vibonde ASFC

Simba, Yanga Waanza Kuweka Viporo Mechi Za NBC Yanga, Simba, Azam zapewa vibonde ASFC

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vigogo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Yanga na Azam wamepewa vibonde katika hatua ya kusaka tiketi ya 32 bora kwenye mashindano ya Kombe la Shikisho la Azam (ASFC).

Katika Droo iliyopangwa leo Novemba 29 imeshirikisha jumla ya timu 64 kusaka taji Azam Sport Federation Cup.

Mabingwa watetezi Yanga watakutana na Haulung ya daraja la kwanza wakati Simba wakiwakaribisha Tembo FC Mabingwa wa Ligi ya Mkoa wa Tabora huku Azam wenyeji wa Alliance kutoka Mwanza

Kwa mujibu wa droo hiyo, mechi 32 za raundi ya tatu ambazo zitachezwa kati ya Desemba 15 hadi 17 mwaka huu ni kama ifuatavyo, Singida Foutain Gate itaikaribisha Arusha City, KMC itacheza dhidi ACA Eagle.

Dodoma Jiji watavaana na Magereza FC, JKT Tanzania watacheza dhidi ya Kurugenzi FC, Kagera Sugar wao watacheza dhidi ya Dar City, Geita Gold watavaana na Singida Cluster, Namungo watacheza dhidi ya Hollywood FC.

Tabora United watavaana na Monduli Coffee ya Arusha, Coastal Union watacheza dhidi ya Greenland FC, Ihefu watakuwa na Rospa FC, Tanzania Prisons dhidi ya TRA Kilimanjaro, Mtibwa Sugar dhidi ya Nyakagwe na Mashujaa FC dhidi ya Mbuga FC

Chanzo: www.tanzaniaweb.live