Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC: Sure Boy Sio wa Majaribio

Sure Neno Yanga SC: Sure Boy Sio wa Majaribio

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetamba kuwa usajili wa dirisha dogo ambao wanaendelea kuufanya sio wa wachezaji wa majaribio, bali wanashusha vyuma kweli ambavyo vinakuja kuingia kwenye kikosi moja kwa moja kuendana na mahitaji ya kocha Nasredine Nabi.

Mpaka sasa kwenye dirisha hili la usajili Yanga wamekamilisha na kumtangaza aliyekuwa kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ambaye amekuwa nyota wa kwanza kutangazwa na timu hiyo.

Mbali na Sure Boy, Yanga pia inatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho za kumalizana na mawinga Denis Nkane wa Biashara United na Mkongomani Chiko Ushindi huku pia makipa Metacha Mnata, Aboutwalib Mshery na Mohammed Makaka wakiwa sehemu ya nyota wanaotajwa kuwa kwenye uwezekano wa kuibukia Jangwani.

Akizungumzia mchakato wa usajili kwenye kikosi chao, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Tunaendelea vizuri na taratibu za usajili wa wachezaji wapya ndani ya kikosi chetu, mpaka sasa tuna nafasi nne za kuongeza wachezaji wapya hasa baada ya kuondoka kwa Ditram Nchimbi na kikosi kusalia na wachezaji 27 pekee.

“Niwahakikishie kuwa tunafanya usajili makini na wa wachezaji ambao si wa majaribio, bali wale ambao wanakuja kuingia kwenye kikosi moja kwa moja na kuonyesha uwezo wao ikiwa mwalimu atawapa nafasi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live