Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC: Leteni yeyote tunapiga

Yanga Mwanza12 Yanga SC: Leteni yeyote tunapiga

Fri, 8 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKURUGENZI Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said, ametamba kuwa wapo tayari kupambana na timu yoyote kwa kikosi walichonacho na kupata matokeo mazuri ya mastaa wao.

Yanga juzi ilishinda mechi ngumu dhidi ya Azam, licha ya kutanguliwa kufungwa bao moja, mwisho ikashinda 2-1, na kama kawaida Fiston Mayele alitetema baada ya kufunga bao la ushindi kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Yanga katika mchezo huo ilikosa mastaa wake watano muhimu na tegemeo ambao ni Khalid Aucho, Feisal Salum, Jesus Moloko, Farid Mussa na Yannick Bangala.

Akizungumza, Hersi alisema kuwa wanajivunia ubora wa kikosi chao cha msimu huu baada ya kufanya usajili wa kisasa wenye hadhi kubwa kitaifa na kimataifa ambao utawapa ubingwa wa ligi. Hersi alisema ubora huo wa usajili ndio unawapa kiburi na jeuri ya kumtumia

mchezaji yeyote pale anapokosekana mmoja katika kikosi cha kwanza kama ilivyojitokeza katika mchezo wao dhidi ya Azam ambao waliwakosa nyota wao wanne tegemeo na wakapata ushindi.

Aliongeza kuwa kutokana na ubora wa kikosi chao, wapo tayari kucheza na timu yoyote hivi sasa huku nguvu wakizielekeza katika michezo miwlii, wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Geita Gold keshokutwa Jumapili na dhidi ya Simba, Aprili 30, mwaka huu.

“Matarajio makubwa ya wapinzani wetu tunaowania ubingwa pamoja walikuwa wakitarajia kuwa tutapoteza mchezo dhidi ya Azam, hiyo ni baada ya kuwakosa wachezaji wetu watano au wanne tegemeo waliokuwepo katika kikosi cha kwanza ambao ni Aucho, Fei Toto, Bangala, Moloko na Farid.

“Lakini walikuwa hawajui ubora wa kikosi chetu kutokana na usajili tulioufanya katika msimu huu, walisahau wapo akina Ngushi (Chrispin), Nkane (Denis), Ambundo (Nickson) na Makambo (Heritier) ambao wana uwezo wa kubadili matokeo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live