Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Ruvu mechi ya kisasi

A017dce7c50ca7fed8412929e0821500 Yanga, Ruvu mechi ya kisasi

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Yanga leo itawakabili Ruvu Shooting katika mchezo wa mzunguko wa 14 utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi sasa ikiwa imecheza 13, imeshinda tisa, sare nne na kufikisha pointi 31.

Pia Ruvu imekuwa katika kiwango bora hivi karibuni ikiwa katika nafasi ya nne kwa pointi 23 baada ya kucheza michezo 13, kushinda sita, sare tano na kupoteza miwili.

Timu hizo zilipokutana msimu uliopita zilifungana, Ruvu mzunguko wa kwanza ilishinda kwenye Uwanja wa Uhuru kwa bao 1-0 na Yanga ikarudisha mzunguko wa pili kwa bao 1-0.

Ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili, Yanga ikitaka kuendelea kujiimarisha kileleni na Ruvu ikitaka kuzidi kupanda katika nafasi za juu. Michezo mingine itakayochezwa leo Mtibwa Sugar dhidi ya Mwadui huko Morogoro na Ihefu dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa Sokoine, Mbeya.

Timu hizi zote kila moja inahitaji matokeo kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo yao yaliyopita na nafasi walizopo.

Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 14 kwa pointi 13 katika michezo 13, Mwadui nafasi ya 17 kwa pointi 10 katika michezo 13, JKT Tanzania ya 16 kwa pointi 10 na Ihefu ikishika mkia kwa pointi sita.

Katika michezo iliyochezwa jana Kagera Sugar iliifunga Tanzania Prisons kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa na Coastal Union ikiwa nyumbani Uwanja wa Mkwakwani ilitoka suluhu na Mbeya City.

Chanzo: habarileo.co.tz