Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princess sasa kishua zaidi

Yanga Princes Kishua Kikosi cha Yanga Princess kikiendelea kujifua

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga jana imelamba mkataba mpya wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh 170 Milioni utakaoenda kuifanya timu ya soka ya wanawake ya klabu hiyo, Yanga Princess kuishua wakati ikisubiri msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL).

Klabu hiyo ilisaini mkataba na kampuni ya Watercom inayozalisha vinywaji baridi ambapo kwa mwaka huo watapewa Sh 120 Milioni pamoja na katoni 1500 kila mwezi kwa wachezaji wa timu hiyo na zile za vijana na wakubwa.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi akizungumza kwenye hafla ya utiliwaji wa saini hiyo, alisema kila mwezi klabu itakuwa inapata Sh 10 Milioni na katoni za vinywaji vyenye thamani ya Sh 50 Milioni na sehemu kubwa itahudumia Yanga Princess iliyomaliza ligi ya msimu uliopita katika nafasi ya tatu.

“Tunategemea mkataba huu utazaa matunda mazuri na tunawatakia kila la heri Yanga kwa mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan utakaopigwa wiki iliyopita,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Watercom, Mohammed Salim.

Chanzo: Mwanaspoti