Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princess na mahesabu ya Ubingwa Ligi ya Wanawake

Kikosi Yanga Princess 1024x732 Kikosi cha Yanga Princess

Sun, 26 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Sare ya bao 1-1 iliyoipata mbele ya watani wao wa jadi Simba Queens katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) imewapa mzuka Yanga Princess na kutangaza kwamba wanautaka ubingwa wa ligi hiyo kutokana na kile ilichodai kwa sasa ni kama hauna mwenyewe.

Yanga ilitoka sare ya aina hiyo ya pili mfululizo msimu huu dhidi ya Simba Queens katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Uhuru na kuifanya ifikishe pointi 22, huku watetezi - Simba wakiishia juu yake nafasi ya tatu na pointi 27, wakati vinara Fountain Princess ikiwa na 29 na JKT Queens ikiwa na 28.

Zikiwa zimesalia mechi sita kabla ya kufungwa kwa msimu, kocha wa Yanga Sebastian Nkoma alisema anaamini ubingwa upo wazi na kama watakomaa watabeba ndoo, huku kocha wa Simba, Charles Lukula akikiri walizembea kuzoa pointi tatu mbele ya watani.

Simba ndio iliyotangulia kupata bao kwenye mchezo huo kupitia kwa Jentrix Shikangwa kabla ya Wogu Chioma kusawazisha, na Lukula alisema hawana wa kumlaumu zaidi ya uzembe.

“Yanga walikuwa wazuri kwenye eneo la kulinda na kuzuia jambo lilifanya wachezaji wangu kukosa nafasi za kupita, lakini nawapongeza pia kwa kujituma japo dakika za mwishoni walichoka,” alisema Lukula, huku Nkoma akisema matokeo hayo hayawazuii wao kupata ubingwa msimu huu kwa kuwa bado wana mechi nyingine.

Chanzo: Mwanaspoti