Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princess mshindi wa Tatu Ngao ya Jamii 2023

Yanga Princess Ngao Ya Jamii Yanga Princess mshindi wa Tatu Ngao ya Jamii

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga Princess imechukua nafasi ya tatu mashindano ya Ngao ya Jamii 2023 baada ya kushinda kwa penalti 4-2 dhidi ya Fountain Gtae Princess baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu 0-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Timu hizo zimecheza mshindi wa tatu baada ya Yanga Princess kufungwa na Simba Queens kwa penati 5-4 mechi ya kwanza (nusu fainali) na Fountain Gate Princess ilifungwa na JKT Tanzania mabao 5-0.

Penati zote nne za Yanga Princess zilipigwa na Precious Christopher, Safiatu Salifu, Cidalia Cuta na Diana Dantwi huku mbili za Fountain zilizoingia kambani zikifungwa na Aquila Gaspar na Hasnath Ubamba na waliokosa ni Zawadi Hamis na Privilege Mupeti.

Michuano hiyo mipya iliyoanza msimu huu inashirikisha timu nne za juu ambazo ni mabingwa wa Ligi Kuu JKT Queens, Simba Queens, Fountain Gate Princess na Yanga Princess.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: