Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princess kuanza msimu leo

Yanga Princess1 Yanga Princess kuanza msimu leo

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu ya wanawake Tanzania Bara inaendelea leo Jumatano, Desemba 7, 2022 kwa michezo 4 kupigwa viwanja tofauti.

Yanga Princess itakuwa wenyeji wa Fountain Gate Princess kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Baobab Queens itakuwa mgeni wa Amani Queens kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Nyangao iliyopo Mtama mkoani Lindi wakati Alliance Girls itakuwa mwenyeji wa Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza.

Nayo The Tigers Queens itakuwa mwenyeji wa Mkwawa Queens kwenye uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu mkoani Arusha.

Ligi hiyo imeanza Desemba 6 kwa mchezo mmoja wa ufunguzi ambapo mabingwa watetezi Simba Queens imeanza kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa JKT Queens.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live