Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princess hawapoi

D80c3ae27a2d2d58351720c091b72db3 Yanga Princess hawapoi

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya soka ya Yanga Princess imezidi kujikita kileleni baada ya kuifunga TSC ya Mwanza kwa mabao 7-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mabao katika mchezo huo yalifungwa na Aisha Khamis alifunga manne, Amina Ally alifunga mawili na Philemona Daniel alifunga moja. Kwa matokeo hayo, Yanga imefikisha pointi 28 baada ya kucheza michezo 10 na kushinda tisa na sare moja.

JKT Queens ikicheza ugenini katika Uwanja wa Nyamagana Mwanza iliwafunga wenyeji Alliance kwa mabao 2-1. Kwa matokeo hayo, JKT imefikisha pointi 24 katika nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 10, ikishinda michezo nane na kufungwa michezo miwili na Alliance inaendelea kubaki katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 19.

Simba Queens ikicheza ugenini katika Uwanja wa Mabatini Pwani iliifunga Mlandizi kwa mabao 2-0 ambayo yalifungwa na Asha Djafari na Oppa Clement. Simba imefikisha pointi 23 baada ya kucheza michezo tisa, ikishinda michezo saba na sare mbili na Mlandizi inaendelea kubaki na pointi zake 11.

Dodoma Baobab iliifunga Tanzanite 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Fountain Gate na kufikisha poibti 19 na Tanzanite ikibaki na pointi 12.

Chanzo: habarileo.co.tz