Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princess: Wananchi watarajie furaha

Yanga Princess Gh Yanga Princess.

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Joha Said ambaye ni Meneja wa Yanga Princess, ameelezea hali ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Soka Wanawake Tanzania Bara.

Ligi Kuu Soka Wanawake Tanzania Bara ikiwa imesimama kwa muda baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza. Yanga Princess yenyewe inaendelea kujifua kuhakikisha ligi itakaporejea inakuwa imara zaidi katika kusaka nafasi ya kwanza.

Akizungumzia hali ya kikosi cha Yanga Princess na kinachoendelea kwa sasa, Joha alisema: “Tangu tumemaliza mzunguko wa kwanza (Februari 8) kikosi kiko vizuri, hakuna majeruhi, kwa ujumla kila kitu kipo sawa tukijiandaa na mzunguko wa pili.

“Kinachoendelea kwa sasa ni mazoezi madogomadogo, tunaendelea kujiimarisha tukiwa na matarajio makubwa sana, tunaenda kuwapa furaha Wananchi, tunaenda kukaa katika nafasi ile tunayoitaka (namba moja).

“Wananchi watarajie furaha kutoka kwa Yanga Princess, kuna maendeleo makubwa sana kwa namna mazoezi yanayoendelea, kwa hiyo kila kitu kitakuwa sawa, tunaenda kukaa katika nafasi yetu sasa.”

Yanga Princess imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya tatu ikikusanya pointi 18 baada ya michezo tisa. Tofauti na vinara ni pointi saba pekee.

Mzunguko wa pili wa ligi hiyo unatarajiwa kuanza Machi 12, mwaka huu ambapo Yanga Princess itacheza mechi yake Machi 13 dhidi ya Baobab Queens.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: