Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princess, Simba Queens hatoki mtu

005b4eb17cc54f8132a42aeebcaf5edf Yanga Princess, Simba Queens hatoki mtu

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Soka la Wanawake kati ya watani wa jadi, Yanga Princess na Simba Queens utachezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku tambo zikitawala kwa pande zote.

Akizungumza na gazeti hili jana, kocha wa Yanga Princess, Edna Lema alisema wamejiandaa vizuri na anachotaka ni mchezo wa kiungwana kwa timu zote tatu. “Yanga Princess na Simba Queens hazijawahi kukutana wakiwa katika msimamo kama wa msimu huu, hivyo matokeo ya kesho (leo) yataleta twasira ya msimu utakavyokuwa,” alisema Edna.

Pia alisema Yanga Princess haijapoteza mchezo hivyo wanastahili kushindania ubingwa na kuchukua ubingwa ni sehemu ya maandalizi ambayo wamefanya kwa ajili ya msimu huu.

Naye kocha wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema hana majeruhi na Yanga Princess anawafahamu mwaka wa tatu sasa ila mwaka huu wameleta uhalisia wa maana ya mechi ya Yanga na Simba ila Simba Queens wana asilimia kubwa ya kushinda.

“Simba Queens hatuna presha yoyote, sisi ni bingwa mtetezi na mshindi wa mchezo wa kesho (leo) Yanga ndio atakuwa kwenye nafasi nzuri, kiufundi Simba tupo vizuri,” alijinasibu Mgosi.

Mgosi alisema kule ambapo Yanga Princess wamepita na kupata matokeo mazuri ndiko Simba Queens anapoelekea na kule ambapo Simba imetoka sare ndipo Yanga wanapoelekea hivyo Yanga sasa wana kazi ngumu.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa Mo Simba Arena timu hizo zilitoka suluhu ukiwa ni msimu wa kwanza kwa Yanga Princess kufuta uteja tangu ipande Ligi Kuu ya Wanawake kutoka kupigwa mabao mengi.

Kwenye msimamo, Yanga Princess inaongoza ikiwa na pointi 38 ikifuatiwa na Simba Queens yenye pointi 36 baada ya kucheza michezo 14 kila moja.

Yanga Princess imeshinda michezo 12 na sare mbili na Simba imeshinda 11 na sare tatu, Simba imefunga mabao 55 na Yanga imefunga mabao 47.

Chanzo: www.habarileo.co.tz