Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princess, Ruvuma Queens mbona kazi ipo

Wanawake+pic Yanga Princess, Ruvuma Queens mbona kazi ipo

Sat, 18 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Mustafa MtupaLIGI Kuu ya Wanawake (SWPL) inaendelea jioni ya leo, lakini kuna kazi nzito kwenye baadhi ya viwanja hasa pambano la Yanga Princess dhidi ya Ruvuma Queens na vinara Simba Queens watakuwa ugenini mjini Kigoma dhidi y Kigoma Sisters, huku maakocha wa timu zote wakitambiana.

Yanga na Ruvuma zitamalizana kwenye Uwanja wa Karume, mechi itakayopigwa kuanzia saa 10 jioni na Kocha wa wageni hao wa ligi kutoka mjini Songea, Mohammed Mwamba ametamba kuwa kwa namna alivyowaandaa vijana wake, haoni kwanini Yanga isipasuke nyumbani..

Ruvuma kwa sasa ipo nafasi ya tatu na pointi zao 35 baada ya kucheza michezo 16 na Kocha Mwamba amesema  kiu yao ni kupata matokeo mazuri ugenini kabla ya kwenda kujiweka sawa nyumbani na kutimiza ndoto zao za kubeba ubingwa unaoshikiliwa na JKT.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini wachezaji wote wapo sawa na kama kocha nimejipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na jambo zuri ni kwamba tayari tupo jijini Dar tukiwa tumejipanga kwa mchezo huo," amesema Mwamba, huku upande wa Yanga wamesisitiza hawana maneno mengi, bali dakika 90 za mchezo ndizoz zitakazothibitisha walivyojiandaa.

Mechi nyingine ya leo itawakutanishaa watetezi wa ligi hiyo iliyoasisiwa mwaka 2016, JKT Queens watakaoliamsha mapema dhidi ya Panama kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, huku kila moja ikisaka ushindi kwa nia ya kujiweka pazuri kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Simba Queens ambao  watakuwa mjini Kigoma kumalizana na wenyeji wao Kigoma Sisters.

Mchezo wa Simba na Kigoma utapigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, huku vinara hao wakiwa kileleni na alama 38 baada ya mechi 16 na wakitoka kugawa dozi nene kwa Marsh Queens.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz