Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princes yaitungua Alliance

Yanga Alliance Yanga Princes yaitungua Alliance

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga Princess, jana kimeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Alliance Girls katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Wanawake na kumaliza mzunguko wa kwanza kibabe.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, Yanga Princess ilitokea nyuma na kupata ushindi huo muhimu.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga Princess ilikuwa nyuma kwa goli 1-0, lakini kipindi cha pili, Madina Traole alifunga goli dakika ya 57, kisha Oluwa Yemis akamaliza kazi dakika ya 60.

Ushindi huo unaifanya Yanga Princess kufikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi tisa za mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: