Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princes wanazitaka alama tatu za Alliance

Yanga Princes Msdu Yanga Princes wanazitaka alama tatu za Alliance

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Keshokutwa Alhamisi, Yanga Princess itapambana na Alliance Girls katika muendelezo wa Ligi Kuu Soka Wanawake, mchezo utakaopigwa Dimba la Nyamagana, Mwanza.

Kuelekea mchezo huo wa raundi ya 9, Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Halubono Charles, amezungumzia maandalizi ya kikosi chake.

“Maandalizi yanaendelea vizuri, timu ipo tayari kwa mechi. Matarajio yetu yajayo ni kupambania mafanikio, tunafahamu tunapokuwa ugenini inakuwa mechi ngumu.

“Lakini tumewaambia wachezaji wetu kuwa na tahadhari, hivyo nafasi yoyote tutakayoipata tuitumie.

“Mabinti wanaendelea kuimarika, kitu ambacho ni kizuri, ninaamini tunakwenda kupata magoli tena kwa sababu tumejiandaa vizuri na kila kitu kinaenda vizuri,” alisema Kocha Charles.

Kwa upande wa Noela Patrick Luhala ambaye ni mchezaji wa Yanga Princess, amesema:

“Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri na tunayasikiliza maelekezo ya walimu wetu pale ambapo tumekosea mchezo uliopita tumesahihishwa na tumeelewa, tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi na tunawaahidi ushindi katika mchezo wetu unaofuatia.

“Kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo unaofuatia na kila mchezaji ana morali na tuna uhakika tutashinda.”

Kuhusu afya za wachezaji, Dokta Nahum Muganda, amesema: “Kwa kweli hali ya kikosi tunamshukuru Mwenyezi Mungu wachezaji wote ni wazima, hatuna majeruhi, kwa hiyo tupo tayari tu kwa ajili ya safari kwenda Mwanza kupambana na Alliance.

“Wachezaji kwa kweli tumewaandaa vizuri, kisaikolojia na kiakili, kwa kweli wapo vizuri.”

Yanga Princess itashuka dimbani ikiwa imetoka kuifunga Geita Gold Queens magoli 2-0 katika mchezo uliopigwa Februari 2, 2024 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: