Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princes kuanza na Baobab Queens

Mzungu Yanga Princesss Yanga Princes kuanza na Baobab Queens

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Yanga Princess, inatarajiwa kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Soka Wanawake Tanzania Bara 2023-2024 kwa kucheza dhidi ya Baobab Queens.

Mchezo huo umepangwa kupigwa Desemba 20, 2023 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambapo Yanga Princess itaanzia ugenini.

Ratiba hiyo iliyotolewa jana, inaonesha Dabi ya Kariakoo ya kwanza itakuwa Januari 03, 2024 ambapo Yanga Princess watakuwa wageni wa Simba Queens, kisha dabi ya pili itapigwa Machi 22, 2024, Yanga Princess wakiwa wenyeji.

Ligi hiyo inayoshirikisha timu 10, inatarajiwa kufikia tamati Mei 17, 2024 ambapo Yanga Princess itamalizia nyumbani kwa kucheza dhidi ya Alliance Girls.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live