Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princes: Tutawapiga Bunda Queens

Yanga Princes Msdu Yanga Princes: Tutawapiga Bunda Queens

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu Wanawake Tanzania Bara dhidi ya Bunda Queens, Kocha Msaidizi wa Yanga Princess, Fred Mbuna, amesema maandalizi yapo vizuri na matumaini ni kuondoka na pointi tatu.

Mchezo huo wa raundi ya saba, unatarajiwa kuchezwa kesho Ijumaa Januari 26, 2024 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

“Namshukuru Mungu tuko salama, kama unavyoona tunaendelea na mazoezi, tunajaribu kuondoa makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita na tunategeneza jinsi ya kupata magoli na matokeo mazuri katika mchezo ujao,” alisema Mbuna.

Kuhusu ahadi kwa Wananchi, Mbuna amesema: “Kwanza tunatakiwa tushikane kwenye mabaya na mazuri kwa sababu ni timu yetu, inabidi tuwe pamoja ili tuweze kuifanikisha timu yetu na tunaahidi mashabiki wasituache waje katika mechi yetu ya tarehe 26 waweze kutusapoti ili tupate pointi tatu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live