Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Pointi 9 kufuzu Robo Fainali CAF

Pacome X Azizi KI Yanga Pointi 9 kufuzu Robo Fainali CAF

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga ili iwe na matumaini ya kufuzu, inatakiwa kushinda michezo miwili dhidi ya Medeama na kufikisha pointi saba, lakini pia ipate ushindi dhidi ya Belouzidad kwenye Uwanja wa Mkapa ambapo itafikisha pointi kumi kwa asili ya kundi itakuwa kwenye wakati mzuri.

Kimahesabu, Yanga itakuwa imejiweka kwenye nyakati nzuri za kufuzu hatua ya robo fainali na itakwenda Misri kumalizana na Ahly bila presha.

Wakati Yanga inacheza na Medeama, kumbuka kuwa Ahly itakuwa ikimalizana na Belouizdad kwenye michezo ya nyumbani na ugenini, kama Ahly itafanikiwa kushinda michezo yote itakuwa imefikisha pointi kumi, ikiwa na uhakika wa kwenda robo, kimahesabu.

Lakini itakuwa imebakiza mchezo dhidi ya Medeama ugenini na Yanga nyumbani ambapo kwa uhakika wa kuongoza kundi itatakiwa kutafuta pointi tatu.

Lakini kama watagawana pointi na CR, kila mmoja akachukua tatu hali hiyo itawalazima Ahly kushinda dhidi ya Medeame ugenini na kufikisha pointi 10 halafu ili wawe na uhakika wa uongozi kwenye kundi itatakiwa kuwafunga Yanga na kufikisha pointi 13, ambapo pia mahesabu yao yatakuwa kwa CR.

Kwa hali ilivyo, kama Yanga itashindwa kukusanya pointi zote sita kwenye michezo yake miwili dhidi ya Medeama, itakuwa na pointi nne na Medeama saba.

Haya yatakuwa matokeo mazuri kwa Medeama kwa kuwa pointi zao saba zitawalazimisha kutafuta pointi tatu kwenye michezo miwili, dhidi ya Ahly na Belouzdad na kufikisha kumi ambazo zitakuwa zinawapeleka na Yanga itatakiwa kuichapa Ahly ugenini na Belouzdad na kufikisha pointi 10 ambazo zitawafanya waangalie walipokutana ‘head to head’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: