Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Pamba ni mechi ya kihistoria

74560 Pamba+pic

Sat, 7 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KESHO Jumamosi historia itawekwa uwanja wa CCM Kirumba pale Pamba FC itakapowakabili Yanga katika mchezo wa kirafiki ikiwa ni miaka 20 tangu timu hizo kukutana.

Yanga kwasasa inajiandaa na mchezo wake Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United utakaopigwa Septemba 14 huku Pamba wakijiwinda na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Mchezo huo unavuta hisia kubwa ikiwa ni muda mrefu tangu kukutana kwa timu hizo mwaka 1999 wakati Pamba ikiwa Ligi Kuu ambapo Yanga ilikubali kulala kwa mabao 3-1 uwanja wa CCM Kirumba.

Katika kujiandaa na mechi ya kimataifa, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema watatumia vyema mechi hiyo ya kirafiki kubaini mapungufu kwenye kikosi chake.

Amesema malengo yao ni kuona Yanga inapata ushindi kwenye mchezo wao na Zesco na kutengeneza mazingira mazuri ya kusonga mbele.

“Tunajiandaa na mechi ya kimataifa dhidi ya Zesco United, ni mchezo mgumu ambao unahitaji maandalizi ili kufikia malengo yetu, tutatumia mechi hiyo kurekebisha mapungufu”alisema Zahera.

Nao nyota wa Pamba wamesema mchezo huo ni muhimu kwao katika kujiweka sawa na Ligi kwani malengo yao ni kupandisha timu Ligi Kuu.

Straika mkongwe wa timu hiyo, Shija Mkina amesema wamejipanga vizuri na wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo ambao utaongeza morari msimu ujao wa ligi hiyo.

“Ni mchezo mzuri na muhimu sana kwetu katika kujiandaa kisawasawa na Ligi, naamini utakuwa ni kipimo tosha kwetu na tunahitaji ushindi ili kuongeza hamasa kwetu na mashabiki," alisema Mkina.

Kiungo Hamis Thabit amesma; "Kwa sasa tunapambana kuipandisha timu Ligi Kuu, hivyo mchezo huo una faida kubwa kwetu,Yanga ni timu kubwa lazima tuheshimu mechi hiyo”alisema Thabit.

Kipa Kelvin Igendelezi amesema kucheza na timu hiyo inayoshiriki michuano ya kimataifa itawapa nguvu na kujiamini kuelekea mashindano yao.

Chanzo: mwananchi.co.tz