Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Ndoto ya Manji inakwenda kutimia hivi karibuni

Manji.jpeg Yusuf Manji

Sat, 6 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga Afrika, Ali Kamwe amesema kuwa ndoto ya mfadhili na Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Yusufu ManJi inakwenda kutimia siku si nyingi.

Amesema Manji alikuwa na ndoto ya kuona Yanga inatwaa ubingwa wa Afrikana kwamba timu hiyo inaendelea kujipanga kutimiza ndoto hiyo. Manji alifariki dunia hivi laribuni nchini Marekani alikokuwa akitibiwa.

Kufuatia kifo hicho, Kamwe ametoa salamu za pole kwa mashabiki wote nawapenzi wa Yanga na kumwombea mapumziko mema huko alikotangulia.

"Kwa nĂ­aba ya viongozi wa Young Africans, kamati ya utendaji yote, sekretarieti, wanachama, mashabiki na wapenzi wa Yanga tumepokea kwa mshtuko sana taarifa ya msiba huus. Sisi Yanga tutaendelea kumwenzi ManJi na tunaomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi," amesema Kamwe.

Kamwe amesema hayo leo Julai 1, 2024 katika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kusherehekea ujio wa Mwamba wa Lusaka, Clatous Chota Chama ambaye Jana alimaliza mkataba wakena Klabu ya Simba na leo ametangazwa rasmi kwa ni 'Mwananchi'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live