Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Mwanachama hai ndiye atapiga picha na Kombe

Yanga Mashabiki Z Mashabiki wa Yanga.

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Wanachama na Masoko wa Klabu ya Yanga SC, Ibrahim Samuel amesema Mwanachama hai wa timu hiyo ndiye atakayepiga picha na kikombe walichokitwaa msimu huu.

Yanga SC jana imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Manungu Complex Jijini Morogoro.

Akiandika katika ukurasa wake rasmi wa Instagram Mkurugenzi huyo aliandika kuwa “ Good morning Wananchi. Leo ndiyo siku pekee nategemea kuona Wana Yanga SC wenye kadi mnalipa ADA zenu kuliko siku yoyote ile ndani ya msimu wa 2023 2024.

“Wale wenye na kadi naendelea kuwakumbusha; Ni wanachama na mashabiki wenye kadi HAI tu ndiyo wataopiga picha na kombe la msimu huu.“

Chanzo: www.tanzaniaweb.live